Oct 30, 2009

NA ELIETH SEKIKU

MAUHAJI YA ALBINO TANZANIA

Ni masikitikitiko makubwa ya mauhaji ya albino ambayo yalitokea katika nchi yetu ya Tanzania na bado yanaendelea ila kwa sasa yamepungua sio kama hapo awali. Na hii inatokana na imani ya kishirikina ambapo mtu anataka utajiri wa haraka kwa kupitia viungo hivyo vya albino au zeruzeru.

Huu ni ukiukaji wa haki za binaadamu,inasikitisha na kutia aibu taifa letu la tanzania hasa kwenye nchi za kigeni,unapoangalia na kusoma vichwa vya habari na mahojiano dhidi ya kuuwawa kwa maalbino nchi tanzania..

Naona kila mmoja wetu itabidi kuwajibika na kulikemea swala hili wazi wazi bila kuoneana aibu,ni fedhea na ukatili usiostahika katika jamii yetu,serikali lazima ichukue hatua kali kwa yoyote yule aanayehusika au kukamatwa kwa kumua albino..hukumu yake lazima iwe ni kunyongwa,bila ya kujali ni nani au anawadhifa gani.

Na katika jamii zetu albino wamekuwa wakikumbana na changamoto mbali mbali kama kunyapaliwa na jamii wanazotokea kuanzia koo zao na hata jamii inayowazunguka na kuwachukulia kama watu wasiokuwa na thamani yoyote kwenye jamii na kulifanya tatizo la mauaji linakomaa, maana wanakuwa hawana watetezi wakaribu.

Hata wanapopatwa na matizo mauaji na vtisho wanakosa msaada wa karibu,kwa ujumla jamii imekuwa haitoi ushirikiano wa kutosha kuhakikisha wale wote wanaohusika na mauaji wanapatikana kupitia ushirikiano jamii.

Wamekuwa wakikosa ulinzi wa kutosha pamoja na siraha maalum za kujilindia maadui wao kama vile visu vya kukunja(okapi)na hata filimbi,filimbi ambazo zilitolewa hazikutosha kuwafikia walemavu wote wa ngozi, na zana nyingine ambazo ni muhimu sana kama vile Bastola zitakazowasaidia sana kupambana na wauaji hawa. Na serikari inabidi iweke ulinzi kamili na kufuatilia kesi zao ziwe na uzito katika ufuatiliaji.

Kukosa wafadhili wa kuwawezesha mitaji ya kuanzisha biashara ndondogo na hii ni pamoja na kukosa ofisi maalum ya kufanyia kazi zao na vifaa vya kutosha vya mawasiliano kama vile Simu, radio na kamera kwa ajili ya kupiga picha mazingira wanayoishi kuwa ni ya hatarishi zaidi na kuwafanya wasioamini kuwa wako kwenye mazingira magumu waweze kuamini haya yanayozungumzwa. Na Elieth Joseph

No comments:

Post a Comment