Jun 5, 2010

JE HAKI YA MWANAMKE IKO WAPI?

Naitwa ELIETH SEKIKU, NI mtangazaji wa Radio Fadeco iliyoko Wilaya Karagwe Mkoa Kagera Tanzani. Katika Radio hii natayarisha kipindi cha jukwaa la Mwanamke ndio maana nimeamua kuleta mada hii ya je haki ya mwanamke iko wapi?

Kuna mambo muhimu ya kuangalia, kama Uzazi, Uongozi, Uridhi, na ukija kufafanua moja moja, nitaanza na Uzazi, nikimaanisha kuwa mwamke ndie anabeba mimba ndie anahangaika baba akiwa kwenye starehe zake na mwanamke akijifungua salama anamshukru mungu, sasa unaanza kulea mtoto analia usiku kucha ni wewe, mtoto anaumwa ni wewe na ukija kuangalia kuna mama wengine bado wanazaa kwa kufatanisha watoto, sasa ukimwambia baba tuzae kwa mpango baba anakataa make kupanga uzazi inabidi mpange nyinyi wawili, ukipanga peke yako akaona unachelewa kuzaa ugonvi hakuna kuelewana ndani ya nyumba, na ukizaa watoto wawili wakawa wasichana ni ugonvi baba anasema misichana imezidi humu nndani mpaka mama anakosa amani huyu mama anakuwa anaweka hizo mimba? Hapo haki iko wapi.

Ukiangalia upande wa uongozi, unakuta wakina baba wanasema eti wao hawawezi kuongozwa na wanawake, ambayo ni dhana potofu na sisi wanawake walitujengea mpaka tukawa na woga tukashindwa kujisimamia sisi kama sisi hii tena ukitaka kuilezea itachukua mda.

Ukija kwenye uridhi wa mali sasa hapo ndo tumeteketezwa jumla, unakuwa na mme wako mnahangaika na kutafuta mali hiyo lakini unakuta ukitaka kuongeza mwanamke mwingine anampachika hapo hapo ukisema anasema eti ni mali yake huwezi kuweka masharti kwani wew uliweka nini hajui bila kuangali hiyo mali mwanamke kama wewe inaweza kuteketea, kuna wanawake fisadi katika familia kila baba akijaribu kuleta maendeleo mama anafilisi tu, na upande mwingine mme wako akifa ndo shemeji zako wanaanza kujitokeza kusudi waweze kukunyanganya kile ulichonacho hawana hata haya wanasema eti ni mali ya ndugu yao na wakumbuke kuwa mtegemea cha ndugu hufa hali maskini. Sasa wapendwa hapo haki ya mwanamke iko wapi? Mimi naona tutazidi kukandamizwa mpaka mwisho hata sheria hazilindi mwanamke kikamilifu.

By Elieth Sekiku.